Published On: Mon, Jun 5th, 2017

ARUSHA YAUNGANA KUADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA

Share This
Tags

Jiji la Arusha limeungana na wadau mbalimbali duniani  kuadhimisha siku ya mazingira  kwa kupanda miti  katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Viongozi wa upandaji wa miti  ni pamoja na diwani  wa kata ya Temi VENANCE KINABO na afisa mazingira wa jiji Arusha FLORA ASEI ambapo wamesema zoezi hilo litakuwa endelevu ili kutunza mazingira hasa katika kukabiliana na mabadiliko tabia nchi.

Maadhimisho hayo yamehitimishwa katika bustani yaTemi ambapo wanafunzi na wadau wengine wameshiriki.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>