Published On: Mon, Jun 12th, 2017
World | Post by jerome

AFUKUZWA KAZI KWA KUKATAA KUPOKEA SIMU YA TRUMP

Share This
Tags

Aliyekuwa mwendesha mashtaka wa juu mjini New York, amefichua kuwa alifutwa kazi na Rais DONALD TRUMP wa Marekani baada ya kupokea simu kadhaa zisizokuwa za kawaida kutoka kwa rais huyo.

PREET BHARARA amesema alihisi simu hizo kutoka kwa Rais TRUMP zilikuwa zimevuka mipaka ya kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu.

BHARARA amesema alifukuzwa baada ya kukataa kuchukua simu ya tatu ya TRUMP.

Hata hivyo Ikulu ya white House haikujibu mara moja madai hayo ya BHARARA.

BHARARA ambaye aliteuliwa na rais mstaafu BARRACK OBAMA na kuhudumu eneo la Manhattan, alisema ilionekana kuwa TRUMP alijaribu kujenga uhusiano fulani baada ya wawili hao kukutana mwaka 2016.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>