Published On: Fri, Jun 30th, 2017

DIAMOND ATAMBULISHA BIASHARA YAKE YA KARANGA

Share This
Tags

Msanii wa muziki wa bongo  Fleva  Diamond Platinumz sasa amepanua biashara yake katika harakati za kuwafurahisha mashabiki na wateja wake.

Msanii huyo alizindua bidhaa ambayo sasa iko madukani nchini Kenya.

Huku wasanii wengi wakitumia muda wao mwingi kuuza tisheti, Diamond alianzisha manukato ya Chibu ambayo ni bidhaa ya kipekee.

Msanii huyo baadaye amefanya  kile ambacho wengi hawakutarajia kwa kuzindua njugu au  karanga siku ambayo alimkaribisha Rayvanny nchini Tanzania.

Hivi ndivyo alivyoandika katika  akaunti yake ya facebook siku ya Alhamisi:

USISEME KARANGA SEMA DIAMOND KARANGA!!!!…Habari njema kwa Vijana wenzangu wote, sasa unaweza kujipatia Mtonyo wa ChapChap kupitia @diamondkaranga ambapo utaweza kununua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa boksi moja lenye pakiti Mia moja (100) ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elfu kumi fanya mawasiliano sasa na mawakala walio karibu yako.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>