Published On: Wed, May 17th, 2017
World | Post by jerome

Zaidi ya watu 100 wauawa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Share This
Tags

Zaidi ya watu 100 wameuawa katika kipindi cha juma moja lililopita kusini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na Umoja wa Mataifa umesema mapigano kati ya makundi ya waasi yanayochochewa na uhasama wa kidini yanasambaa. 

Mapigano yalizidi kupamba moto siku ya Jumatatu katika mji wa Bria ulioko kilomita 300 kutoka kwa mji wa mpakani wa Bangassou na kuwalazimu kiasi cha raia 1,000 kutafuta hifadhi katika kambi za Umoja wa Mataifa.

Hospitali ya shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres MSF iliyoko Bria, kufikia jana ilikuwa imepokea watu 24 waliojeruhiwa huku mapigano yakiendelea.

Mkuu wa MSF katika Jamhuri ya Afrika ya Kati Frederic Lai Manantsoa amesema imekuwa vigumu kuthibitisha idadi kamili ya waathiriwa kutokana na ghasia zinazoendelea na kuwa eneo hilo ni vigumu kulifikia.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>