Published On: Fri, May 5th, 2017

ZAIDI YA WAKIMBIAJI 1,000 KUSHIRIKI DASANI MARATHON

Share This
Tags

Zaidi ya wakimbiaji elfu moja wanatarajiwa kushiriki mbio za DASANI MARATHON jijini Dar es Salaam ambazo zimeandaliwa na Klabu ya michezo ya riadha ya Dar Es Salaam na kudhaminiwa na kampuni ya maji ya DASANI kwa kushirikiana na kampuni ya COCACOLA.

Akizungumza wakati wa kutambulisha mbio hizo Rais wa Klabu hiyo GOODLUCK ELVIS amesema mbio hizo zilizoanzishwa miaka mitatu iliyopita zimekuwa zikiendelea kupata umaarufu mwaka hadi mwaka.

Kwa upande wake Mwanariadha mkongwe JUMA IKANGAA ambaye ametajwa kuwa mgeni rasmi katka ufunguzi wa mbio hizo amesema matarajio yake ni kuona vijana wapya wakiibuka kwenye mchezo wa riadha na kuvunja rekodii mbalimbali walizowahi kuweka.

Washiriki wote katika mbio hizo wanatarajiwa kupata mabegi, T shirt, Medali huku gharama za kujisajili ikiwa ni shilingi elfu 30.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>