Published On: Wed, May 17th, 2017

Wazabuni waliochapisha na kusambaza Vitabu shuleni watakiwa kuwa wavumilivu

Share This
Tags

Serikali imewasihi Wazabuni waliotoa huduma ya chakula katika Shule za Sekondari za Bweni na waliochapisha na kusambaza Vitabu shuleni kuwa wavumilivu wakati ikifanya utaratibu wa kuwalipa deni la shilingi Billion 51.54 wanalodai.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI SELEMANI JAFO ametoa taarifa hiyo Bungeni mjini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum BERNADETA MUSHASHU.

Mbunge huyo alitaka kujua fedha wanazodai Wazabuni na ni lini zitalipwa na serikali ambapo naibu waziri JAFO amesema kuwa deni hilo litalipwa kwa awamu kadri ya uwezo kulingana jinsi serikali itakavyokuwa inapata fedha.

Majibu hayo yalionekana kutowaridhisha baadhi ya wabunge ambapo mbunge wa viti maalum SIKUDHANI CHIKAMBO akaitaka serikali kusema muda maalumu ambao madeni hayo yatalipwa kwani yamekuwa ya muda mrefu swali ambalo limejibiwa na naibu waziri wa fedha na mipango ASHATU KIJAJI.

Katika hatua nyingine waziri wa mambo ya ndani ya nchi MWIGULU NCHEMBA amekiri kuwepo kwa askari wa jeshi magereza wanaokiuka baadi ya haki za wafungwa kutokana na ufinyu wa bajeti na msongamano wa wafungwa.

Waziri MWIGULU ametoa taarifa hiyo wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalum DEVITHA MINJA lililohoji lini serikali itakarabati magereza nchini ili kulinda haki za wafungwa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>