Published On: Wed, May 17th, 2017

Wavulana huenda wakaruhusiwa kuvalia sketi shuleni.

Share This
Tags

Wavulana katika shule moja ya kibinafsi kaskazini mwa jiji la London huenda wakaruhusiwa kuvalia sketi iwapo sheria mpya kuhusu sare ya shule zitaidhinishwa.

Shule hiyo ya Highgate inapanga kuruhusu wanafunzi kuvalia sare yoyote ile ambayo wanataka bila kujali jinsia.

Wamechukua hatua hiyo baada ya kugundua watoto wengi wanauliza maswali kuhusu jinsia yao.

Aidha, hakutakuwa na michezo tofauti ya wasichana na wavulana.

Wasichana katika shule hiyo kwa sasa huruhusiwa kuvalia sare ya wavulana – suruali za rangi ya kijivu, jaketi za rangi ya buluu iliyokolewa na tai.

Lakini wavulana hawaruhusiwi kuvalia sketi za rangi ya kijivu ambazo huvaliwa na wasichana pekee, lakini sasa wataruhusiwa sheria mpya kuhusu mavazi shuleni humo itakapopitishwa.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Adam Pettitt amesema wazazi watashauriwa kabla ya mabadiliko hayo kuanza kutekelezwa.

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>