Published On: Mon, May 15th, 2017
Business | Post by jerome

WATANZANIA WASHAURIWA KUTOTEGEMEA AJIRA PEKE YAKE.

Share This
Tags

Watanzania wameshauriwa  kutotegemea kazi moja ya kuajiriwa  badala yake washiriki shughuli za kilimo ili kujijengea mazingira bora yatakayowasaidia  pindi mtu anapostaafu au kuachishwa kazi.

Kauli hiyo imetolewa na  mratibu wa semina ya wakulima na wajasiriamali wa kanda ya kaskazini LOMAIANI LAIZER iliyofanyika katika ukumbi wa YDCP jijini Tanga kufuatia wananchi kukumbwa katika wimbi la  vyeti bandia na kujikuta hawajui pa kuelekea.

Aidha LOMAIANI LAIZER  amesema imekuwa kawaida kwa baadhi ya wafanyakazi kuona kilimo ni jukumu la watu waishio vijijini na kusahau kuwa ajira ina kikomo huku akiwasisitizia wakulima na wataalamu kuacha kilimo cha mazoea na kuwataka wabadilike kulingana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Licha ya  waajiriwa kushauriwa  kujihusisha na kilimo, wakulima WILLIAM RAPHAEL  katika ufafanuzi wake amesema sekta ya kilimo nayo haiko salama kwani wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa mbegu, pembejeo za kilimo na ukosefu wa masoko.

LUCY MELAKITI ni mwalimu wa shule ya msingi Kisosora jijini Tanga, ambaye ameshiriki katika semina hiyo na kusema elimu hiyo itasaidia  kuwakwamua yeye mwenyewe na wanafunzi anaowafundisha.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>