Published On: Wed, May 17th, 2017

Wakulima walalamikia kupigwa na jeshi la polisi wakidai kusingiziwa wizi.

Share This
Tags

Wakazi wa Jengwe Kata ya Kitanga Halmashauri ya Kasulu Mkoani Kigoma wamelalamikia kupigwa na askari wa jeshi la polisi na kuwaweka kituoni kwa muda mrefu kwa madai ya wizi.

Wakazi hao wamedai kulipishwa faini kwa makosa ambayo hawakuyatenda wakati wamewakamatwa katika Mashamba yao ya Mpunga wakiendelea na shughuli za uvunaji wa mpunga huo licha ya eneo hilo kuwa na mgogoro kati ya  wakazi hao na halmashauri ya kasulu kwa takriban miaka tisa sasa.

Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wakuilma na Wafugaji (RIPAFO) lenye Makao yake Makuu mkoani Tabora Joseph Zengo Paroko, amewataka wakazi hao kuwa wavumilivu kwa kuwa Shirika hilo linashughulikia Mgogoro Huo.

Kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Naibu Kamishina wa Polisi Ferdinand Mtui,akizungumza kwa njia ya simu amesema hajawaagiza askari hao kufanya Ulinzi katika eneo hilo na kuwa hana taarifa juu ya jambo hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>