Published On: Wed, May 17th, 2017

Vijana mkoani Njombe waiomba serikali kudhibiti utapeli unaoendelea katika usajili wa kujiunga na jeshi la wananchi

Share This
Tags

Wananchi mkoani Njombe wamelalamikia kuibuka kwa matapeli wanaojikusanyia pesa kwa njia ya udanganyifu kwa vijana wanaohitaji kujiunga na jeshi la wananchi Tanzania wakidai  kuwasaidia kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo.

Uvumi wa kutangazwa kwa nafasi hizo umeibuka hivi karibuni mkoani Njombe  na kuibua sintofahamu kwa wahitaji  baada ya kuonekana taarifa hizo si za kweli.

Sambamba na hilo wananchi hao wameitaka serikali kuhakikisha usajili wa mwaka huu unasimamiwa ipasavyo ili kuepusha utapeli ambao hutokea kila mwaka ukihusishwa na baadhi ya maafiasa wa jeshi na watumishi wengine wa serikali.

Taarifa za Kuwepo Kwa Nafasi za Kujiunga na Jeshi la Wananchi Wilayani Njombe, zimeishtua Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kulazimika Kutoa Tamko Kali Dhidi ya Watakaobainika Kuhusika na Vitendo Hivyo kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>