Published On: Wed, May 10th, 2017
World | Post by jerome

Trump amfuta kazi mkurugenzi wa FBI James Comey

Share This
Tags

Rais Donald Trump amemfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI kutokana na hatua yake ya kuliangazia suala la barua pepe za aliyekuwa mgombea wa uraisi wa chama cha Democrat Hillary Clinton, mamlaka imesema.

Ikulu ya Whitehouse iliishangaza Washington kwa kutangaza kwamba James Comey amefutwa kazi.

Hatua hiyo inajiri baada ya kubainika kwamba Comey alitoa habari za uongo kuhusu barua pepe za Clinton kwa bunge la Congress wiki iliopita.

Rais Trump aliandika barua kwa bwana Comey kwamba alikubaliana na mapendekezo ya mwanasheria mkuu Jeff Sessions kwamba ameshindwa kuliongoza vizuri shirika hilo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>