Published On: Tue, May 16th, 2017
Business | Post by jerome

TradeMark East Africa Yaboresha Biashara Zanzibar, Yawezesha SMS Kutumika kutoa Vyeti au Kutuma Malalamiko

Share This
Tags

Taasisi ya Trademark East Africa, imeiwezesha zanzibar kuongeza ufanisi wa kibiashara kwa kutumia mfumo wa sms za simu za mkononi, kusajili vyeti vya uhalisia wa bidhaa, na pia kutoa taarifa za vikwazo vya kibiashara ili viweze kushughulikiwa kwa haraka zaidi.

Mfumo huo, umezinduliwa rasmi jana mjini Zanzibar  na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko Zanzibar Ali Bakari Ali, kwa ushirikiano na  Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda na wakulima cha Zanzibar (ZNCCIA) Munira Humoud na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa, Tawi la Tanzania, Bw. John Ulanga.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa TMEA, Tawi la Tanzania, John Ulanga amesema, wanalengo la kuboresha mazingira ya kufanya biashara Zanzibar na hivyo kukuza biashara  na kuleta ufanisi wa biashara na nchi nyingine”.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCCIA, Munira Humoud amesema mifumo hii miwili muhimu itaongeza ushindani visiwani Zanzibar kwenye biashara ya kimataifa kwa kuongeza kasi ya usajili wa vyeti vya uasili na kupunguza vikwazo vya kibiashara, kufuatia vikwazo hivyo kushughulikiwa mapema baada ya taarifa kupokelewa kupitisa SMS.

TMEA imegharimia gharama zote za mradi huo, ambapo, ZNCCIA imefaidika kwa kupatiwa vifaa vya ICT vya kutekeleza mfumo, vifaa vya nishati ya jua kama nishati mbadala pale umeme unapokatika, na kupatiwa  mshauri elekezi  kuratibu mradi huo na misaada ya kiufundi kiuendeshaji.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>