Published On: Fri, May 5th, 2017
Sports | Post by jerome

TALII TANZANIA YAZINDULIWA

Share This
Tags
Bodi ya Utalii nchini TTB, imezindua kampeni maalum ya majuma mawili  ijulikanayo kama ‘Talii Tanzania’ambayo itahusisha mikoa minne ya Kigoma, Dodoma, Mbeya na Mwanza, yenye lengo la kuhamasisha utalii wa ndani.
 
Mkoa wa Kigoma, umepata heshima ya kuzindua kampeni hiyo ambapo Afisa Uhusiano Mkuu wa Bodi ya Utalii nchini, Geofrey Tengeneza, amesema kuwa kampeni hiyo inafuatia kampeni ya waandishi wa habari ambayo CLOUDS MEDIA, kupitia kipindi cha 360, walitembelea hifadhi za Ngorongoro na Serengeti ili kujionea vituo vilivyopo na kuvitangaza.
 Amesema katika kampeni mpya ya Talii Tanzania, wananchi wanafuatwa walipo na kupewa elimu juu ya umuhimu wa wao kufanya utalii wa ndani ambapo maswali mbali mbali huulizwa na wananchi na pia wao kuulizwa kuhusu uelewa wao juu ya utalii wa ndani na zawadi hutolewa.
Wakati huo huo Geofrey Tengeneza, amewatoa hofu wananchi wanaodhani kwamba gharama za kufanya utalii ni kubwa hivyo kuona kuwa utalii ni suala la wazungu pekee.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>