Published On: Wed, May 17th, 2017
World | Post by jerome

Serikali ya Kenya yashusha bei ya unga wa mahindi, wapenzi wa Ugali wafurahi

Share This
Tags

Serikali ya Kenya imetangaza kushusha bei ya unga wa mahindi baada ya kununua kiasi kikubwa cha mahindi kutoka nchini Mexico wiki hii.

Kuanzia siku ya Jumatano, mifuko miwili ya unga itauzwa madukani kwa bei ya Shilingi 90 za nchi hiyo karibu Dola 1, na kuwapa afueni kubwa raia wa nchi hiyo.

Waziri wa Kilimo nchini humo Willy Bett ameeleza kuwa mfuko mmoja wa unga utauzwa kwa bei ya Shilingi 47, hatua ambayo imekubaliwa kati ya serikali na wasagaji unga.

Kupanda marudufu kwa bei ya mahindi ya kusaga na unga wa ugali, limekuwa suala tata nchini Kenya na kuzua mvutano wa kisiasa kati ya serikali na upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti.

Mgombea urais kupitia muungano wa upinzani NASA Raila Odinga, amekuwa akihoji ni kwanini serikali ya rais Uhuru Kenyatta ilisubiri kumalizika kwa hifadhi yote ya mahindi katika maghala ya serikali kabla ya kuamua kununua tani 29,900 katika dakika za mwisho.

Hata hivyo, rais Uhuru Kenyatta ametetea hatua hiyo na kueleza kuwa sababu kuu ilikuwa ni kwa sababu walitoa nafasi kwa wakulima wa ndani kuiuzia serikali mahindi yao kabla ya kwenda nje ya nchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>