Published On: Fri, May 19th, 2017

SERIKALI YA KANUSHA KUHUSU UPUNGUFU WA CHAKULA KWA MAHABUSU

Share This
Tags

Serikali Kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imekanusha Kutokuwa na Tatizo la Upungufu wa Chakula kwa Mahabusu Wanaoshikiliwa Kwenye Vituo vya Polisi pamoja na Magereza Katika Visiwa vya Zanzibar.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU NCHEMBAametoa kauli hiyo Mapema leo Bungeni Mjini Dodoma wakati wa Kipindi cha Maswali na Majibu.

Akijibu Swali la Mbunge wa Chumbwini, USSI SALUM PONDEZA, Waziri NCHEMBA, amesema Serikali imekuwa ikipeleka Chakula hicho Kulingana na Idadi ya Mahabusu Wanaoshikiliwa Kwenye Vituo Hivyo.

 

Waziri Mwigulu ameongeza Kuwa Serikali imekuwa ikizingatia Misingi ya Utawala Bora, Haki za Binadamu pamoja na Utu Katika Kushughulikia Makosa yanayohusu Uvunjifu wa Sheria na Kanuni Mbalimbali.

Katika Hatua Nyingine Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi WILLIAM OLE NASHA amesema Serikali imeendelea Kuchukua Hatua Madhubuti ya Kuboresha Mazingira ya Ukuaji wa Sekta ya Ushirika hapa nchini.

Naibu Waziri Huyo wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Akijibu Swali la Mbunge wa Vit Maalum SHALLY RAYMOND amesema hatua hizo ni kuimarisha tume ya  Maendeleo ya Ushirika, Sambamba na Kuongeza Idadi ya Maofisa Ushirika katika Ngazi ya Taifa.

 

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi leo imewasilisha Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi Kwa Mwaka Ujao wa Fedha, Ikiomba Kuidhinishiwa Kiasi cha Shilingi Bilioni 267.8.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>