Published On: Mon, May 15th, 2017
Business | Post by jerome

SALIM KIJUU: MARUFUKU KUVUSHA KAHAWA KWENDA NCHI JIRANI KIMAGENDO

Share This
Tags

Mkuu wa mkoa wa Kagera  meja jenerali mstaafu SALUM  KIJUU, amewataka viongozi  kuanzia ngazi za vijiji  mkoani humo, kudhibiti na kutoruhusu biashara ya magendo ya kahawa kutokana na biashara hiyo kudidimiza uchumi wa wakulima pamaoja na uchumi wa taifa kiujumla .

Akizungumza  katika kikao cha wadau wa kahawa mkoani humo Mkuu huyo wa mkoa KIJUU amelaani vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu ambao hupitisha zao kwenda nchi  jirani  hali inayopelekea  upotevu wa mapato nchini.

Kwa upande wake Meneja wa bodi ya kahawa mkoani Kagera MERICKED MASSAWE amesema kuwa  kwa msimu ulioanzia mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu, uzalishaji wa zao la kahawa umeshuka ukilinganisha na makadirio ya msimu uliopita.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>