Published On: Wed, May 17th, 2017

Rais Magufuli amteua Geoffrey Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa TIC

Share This
Tags

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Geoffrey Idelphonce Mwambe kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Kabla ya Uteuzi huo  Geoffrey Idelphonce Mwambe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.

Nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Manyoni itajazwa baadaye.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Clifford Tandari kuwa KatibuTawala wa Mkoa wa Morogoro.

Clifford Tandari anachukua nafasi ya Dkt. John Ndunguru ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo Clifford Tandari alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC).

Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>