Published On: Mon, May 15th, 2017
Science | Post by jerome

NISHATI YA UMEME JUA YAWA MSAADA VIJIJINI

Share This
Tags

Wakati serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha nishati ya umeme inaenea katika maeneo yote nchini hasa vijijini , suala la upatikanaji wa nishati ya umeme  jua yaani Solar Power  limeendelea kuwa mkombozi kwa wananchi hasa wa kipato cha chini kwa kuwawezesha kumudu gharama za kuunganishwa na nishati hiyo.

Kupatikana kwa nishati hiyo hadi vijijini kumekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kwa ajili ya matumizi ya nyumbani sambamba na  wanafunzi wa shule zilizopo vijijini kwa ajili ya kujisomea, lakini pia kwa wajasiriamali wadogo ambao wanarahisishiwa namna ya kuendesha biashara mbalimbali ikiwemo vinjwaji baridi.

Kampuni ya nishati ya umeme jua ya  Zola (Zola Power) imeamua kuhakikisha wanawafikia wananchi waliopo maeneo ya  vijijini na mijini na kutoa huduma hiyo kwa bei nafuu.

Kampuni hiyo ya Zola mpaka sasa imeshawaunganisha watu zaidi ya laki mbili na nusu huku kwa mkoa wa Morogoro pekee ikiwa imewafikia  watu zaidi ya elfu nane na mia sita.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>