Published On: Wed, May 10th, 2017
World | Post by jerome

Msichana wa Chibok akataa kurudi nyumbani

Share This
Tags

Mmoja wa wasichana wa Chibok waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram nchini Nigeria ameamua kusalia na mumewe badala ya kuachiliwa huru kulingana na msemaji wa rais wa Nigeria.

Alitarajiwa kuwa miongoni mwa kundi la wasichana walioachiliwa siku ya Jumamosi.

Garba Shehu aliiambia runinga moja kwamba wasichana 83 walitarajiwa kuachiliwa huru lakini mmoja wao akasema : hapana nafurahi nilipo, nimepata mume.

Wasichana 82 waliachiliwa huru ikiwa ni kati ya mazungumzo yalioafikiwa na shirika la ICRC.

Serikali ilikubali kuwaachilia huru wanachama wanne wa Boko haram kubadilishana na wa wasichana hao.

Wapganaji hao wanadaiwa kuwazuilia zaidi ya wasichana 100 kati ya 276 waliowateka katika eneo la Chibok miaka mitatu iliopita.

Kundi hilo pia limewateka maelfu ya raia wakati wa operesheni zao katika eneo hilo.

Inaaminika kwamba baadhi ya wale waliotekwa wameolewa na wapiganaji hoa na wamepata watoto nao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>