Published On: Fri, May 19th, 2017

MJADALA KUHUSU BAJETI WAENDELEA DODOMA

Share This
Tags

 

Wakati Bunge likiendelea na Mjadala Kuhusu Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mjini Dodoma, Serikali imeshauriwa Kuvipa Nguvu Viwanda vya Ndani ili Kupunguza Uwezekano wa Tanzania Kuendelea Kuwa Dampo la Bidhaa Zilizo chini ya Kiwango.

 

Mjadala huo umeingia Siku ya Pili,  ambapo Wabunge wameendelea Kutoa Maoni yao Kuhusu Mpango wa Makadirio ya Mapato na Matumizi wa Wizara ya Hiyo, Uliowasilishwa Jana na Waziri CHARLES MWIJAGE.

Wabunge hao GIMBI MASABA na STANSLAUS MABULA, Wakichangia Mwelekeo wa Bajeti ya Wizara ya Viwanda, wakatumia muda huo kuweza kuishauri  serikali wakitaka  Uwekezaji wa Viwanda Ulenge Kwenye Maeneo yenye Uhakika wa Malighafi, ikiwemo zile za Kilimo na Mifugo.

 

Kando ya Mjadala huo, Mbunge wa Pangani JUMAA AWESO, akizungumza na CLOUDS TV, amesema ili Kuviimarisha Viwanda vya ndani, Serikali inapaswa Kuja na Sheria ya Kudhibiti Uingizaji holela wa Bidhaa toka Nje ya Nchi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>