Published On: Tue, May 16th, 2017

Matumizi holela ya dawa yawaathiri akina mama Kata ya Ndanda, Mtwara.

Share This
Tags

Baadhi ya akina mama katika kata ya Ndanda, halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamekiri kupatwa na madhara kutokana na matumizi holela ya dawa wanazonunua katika maduka ya madawa, jambo linalosababishwa na kukosekana kwa Zahanati katika kata hiyo.

Akina mama hao wamedai kutokana na kuwa na kipato cha chini wanashindwa kumudu gharama za kutibiwa katika hospitali ya rufaa ya Ndanda, hivyo uwepo wa Zahanati ya kata ungekuwa ni msaada mkubwa kwao.

Costansia Ng’ombo ni diwani wa kata hiyo, ambae amekiri kuwapo kwa changamoto hiyo kwa wananchi wake.

Licha ya ujenzi wa Zahanati, mkakati uliopo katika halmashauri hiyo ni kujenga kituo cha afya katika kata ya Chikukwe pamoja na kupandisha hadhi zahanati ya Nangoo kuwa kituo cha afya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>