Published On: Wed, May 17th, 2017

Makamu wa rais awataka polisi wanawake kuonyesha uwezo wao ili waweze kupandishwa vyeo na kupata nafasi za uongozi.

Share This
Tags

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan amewataka askari polisi wanawake kutoka kwenye Shirikisho la Majeshi ya Polisi Kusini mwa Afrika (SARPCCO) washiriki kikamilifu katika oparesheni mbalimbali ambazo zinafanyika kwenye ukanda huo kama hatua ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Makamu wa Rais ametoa kauli hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku Tatu ya Polisi wanawake kutoka nchi wanachama wa SARPCCO Jijini Dar es Salaam na kuwahimiza  askari polisi wanawake kufanya kazi kwa bidii na kujituma hatua ambayo itasaidia kupanda vyeo kama  askari wanaume katika maeneo yao ya kazi.

Amesisitiza kuwa muda wa kulalamika hawapandishwi vyeo umeshapitwa na wakati bali kwa sasa wachape kazi na waonyeshe kuwa wanaweza majukumu yao wanayopangiwa ili waweze kupanda vyeo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Hamad Masauni amesema ana imani kubwa kuwa mafunzo hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa polisi hao wanawake kuimarika ipasavyo katika utendaji wao wa kazi.

Masauni pia amewahimiza polisi wanawake wanaopata mafunzo hayo kwenda kuwaelimisha na wenzao mipango na mikakati waliyoweka katika kulinda raia na mali zao katika nchi zao.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>