Published On: Mon, May 15th, 2017
World | Post by jerome

KOREA KASKAZINI YAFANYA TENA MAJARIBIO YA KOMBORA

Share This
Tags

Korea Kaskazini imedai kwamba kombora la masafa marefu ililolifanyia majaribio jana ni kombora jipya linaloweza kubeba kichwa cha nyuklia.

Kombora hilo lililorushwa lilienda angani kwa urefu wa kilomita 2,000 na kusafiri kilomita 700 kabla ya kuanguka katika bahari Magharibi mwa Japan.

Jeshi la Korea Kusini limesema halijaweza kuthibitisha madai hayo ya Korea Kaskazini, lakini lilionekana kuweza kuruka angani, hatua ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa makombora ya masafa marefu.

Majaribio ya mara kwa mara ya makombora ya masafa marefu yanayofanywa na taifa hilo yanakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa na yamesababisha wasiwasi miongoni mwa jamii ya kimataifa pamoja na Marekani.

Marekani na Japan zimetaka kufanyika kwa mkutano wa dharura katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kesho.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>