Published On: Wed, May 17th, 2017
World | Post by jerome

Kikwete kuhudumu katika baraza la wakimbizi duniani

Share This
Tags

Rais mstaafu wa Tanzania  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, taarifa kwa vyombo vya habari ilimtaja rais Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa masuala ya kigeni nchini Canada, Lloyd Axworthy.

Gazeti hilo limesema kuwa Hina Jinali kutoka Pakistan na Rita Sussmith kutoka Ujerumani watafanya kazi pamoja na Kikwete kama wenyekiti wenza huku Paul Heinbecker akichaguliwa kama naibu na Fen Hamson akihudumu kama mkurugenzi.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>