Published On: Wed, May 17th, 2017
Business | Post by jerome

Kenya-Mauzo ya chai Uingereza yashuka baada ya nchi hiyo kujitoa umoja wa ulaya

Share This
Tags

Kenya hivi sasa inashuhudia athari za Uingereza kujitoa kwenye nchi zinazotumia sarafu ya Euro kufuatia kupungua kwa kiwango cha chai kinachonunuliwa na Uingereza wakati nchi za ulaya zikiamua kuipa kisogo Uingereza na kuagiza bidhaa hiyo moja kwa moja.

Ripoti ya utendaji wa sekta ya chai iliyotolewa na Mkurugenzi wa chai inaonyesha kuwa kiwango kilichonunuliwa na Uingereza kilipungua kutoka kilo 5.4milioni mwezi Machi mwaka jana hadi kilo 3.1milioni kipindi kama hicho mwaka huu.

Kurugenzi ya chai inaonyesha kuwa Uingereza hainunui tena chai kwa kiwango kikubwa kutoka Kenya kutokana na kupungua kwa soko la uuzaji katika nchi nyingine za ulaya ambazo zimekuwa zikinunua bidhaa hiyo kutoka Uingereza.

Mkuu wa kurugenzi ya chai Samuel Ogola amesema kupungua huko kumesababishwa na Brexit,kwani Uingereza ilikuwa mnunuzi mkubwa wa chai ya Kenya ambayo ilikuwa ikinunua kwa matumizi ya nyumbani na pia kuuza kwa nchi nyingine za ulaya.

Mwaka jana wataalam walionya kuwa kujiondoa kwa Uingereza kutoka kwa Umoja wa Ulaya kutasababisha kushuka kwa kiwango cha chai ambacho Uingereza inaagiza kutoka Kenya kutokana na kushuka kwa masoko yake ambayo huuza chai hiyo.

Uingereza ni muuzaji mkubwa wa chai ya Kenya ambapo Mwkaa 2014 iliuza asilimia 17 ya bidhaa hiyo iliyoagiza kutoka Kenya kwa mataifa ya Ireland,Ujerumani,Poland na Ufaransa ambayo ndio masoko yake makubwa.

Ogola amesema nchi ambazo zilikuwa zikinunua chai ya Kenya kutoka Uingereza hivi sasa zinanunua moja kwa moja kutoka Kenya.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>