Published On: Mon, May 15th, 2017
World | Post by jerome

JULIO BORGES ALITAKA JESHI LA VENEZUELA KUANZISHA MAZUNGUMZO

Share This
Tags

Spika wa Bunge lenye wapinzani wengi nchini Venezuela, JULIO BORGES amelitaka jeshi la nchi hiyo kuanzisha mazungumzo na kusaidia kupata suluhu ya mgogoro wa kisiasa.

Jeshi linamtii rais wa nchi hiyo NICOLAS MADURO ambaye amekuwa akipinga shinikizo la upinzani kuitisha uchaguzi mapema.

BORGES amemtaka waziri wa ulinzi, VLADMIR PADRINO LOPEZ kukutana na viongozi wa upinzani na kusikiliza hoja zao.

Amesema jeshi halitakiwi kuegemea upande mmoja na kwamba kazi yake ni kutetea katiba ya Venezuela, ambayo upinzani imesema inatishiwa.

Mapema mwezi huu Rais MADURO alitangaza mipango ya kuunda bunge jipya kwa ajili ya kuandika katiba mpya.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>