Published On: Mon, May 1st, 2017
Sports | Post by jerome

BAHATI NASIBU YAMTOA

Share This
Tags

Mkenya aliyefanikiwa kubashiri kwa ufasaha matokeo ya mechi 17 mwishoni mwa wiki amejishindia jumla ya shilingi bilioni mia mbili na ishirini na moja za Kenya, ambazo ni sawa na dola milioni mbili nukta mbili za Marekani.

Kwa mujibu wa BBC Swahili, kijana huyo wa umri wa miaka 28 ambaye ni mzaliwa wa Kakamega, magharibi mwa Kenya ndiye wa kwanza kujishindia kiasi kikubwa hivyo cha pesa.

Mshindi huyo wa Mega Jackpot ya kampuni ya Sportpesa alianza kushiriki mashindano ya bahati nasibu ya kubashiri matokeo mwaka jana baada ya kutambulishwa kwa mchezo huo na nduguye.

Taarifa zinasema yeye ni mzaliwa wa pili kutoka mwisho katika familia yenye watoto 12.

Amekuwa akiishi katika mtaa wa Eastlands, Nairobi kwa jamaa yake lakini kwa sasa amepelekwa eneo salama kutokana na wasiwasi kwamba huenda watu wakafika kwa wingi kumpongeza au pengine kutaka kufahamu siri yake.

Kijana huyo alikuwa tayari ameanza kusherehekea alipogundua kwamba alikuwa amebashiri vilivyo matokeo ya mechi 14 kati ya 17 zilizokuwa kwenye Mega Jackpot pale alipopigiwa simu na afisa mkuu mtendaji wa Sportpesa Ronald Karauri muda mfupi baada ya saa sita usiku.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>