Published On: Fri, May 19th, 2017

122.2 BILIONI ZA MAKADIRIO YA BAJETI YA WIZARA YA VIWANDA,BIASHARA NA UWEKEZAJI YAPITISHWA

Share This
Tags

 

Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya viwanda biashara na uwekezaji iliyoomba kuidhinishiwa shilingi billion 122.2 kwa mwaka wa fedha 2017/18.

Wakati wakichangia mjadala wa bajeti hiyo baadhi ya wabunge wameitaka serikali kuacha siasa katika swala la viwanda kwani linahitaji utaalamu wa kutosha ili kufikia uchumi wa viwanda, Wabunge hao HUSEN BASHE mbunge wa nzega mjini na mbunge wa mbunge wa kilolo VENANCE MWAMOTTO.

 

Mbunge wa hanang’ MERRY NAGU na MATHA UMBULA mbunge wa viti maalumu wakati Wakichangia bajeti hiyo Wamesema kama mipango ya uanzishwaji wa viwanda itatiliwa mkazo itapunguza migogoro ya wakulima na wafugaji inayosababusha vifo.

 

Akihitimisha hoja ya bajeti yake waziri wa viwanda biashara na uwekezaji CHALES MWIJAGE amesema mfumo wa sasa wa kushugulikia viwanda vilivyobinafsishwa ambavyo havifanyi kazi ili kuvifufua kwa haraka.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>