Published On: Thu, Apr 27th, 2017

ZAO LA TUMBAKU SI NEEMA TENA MKOANI TABORA

Share This
Tags

Kilimo cha zao la Tumbaku Mkoani Tabora kimegeuka kuwa janga la uharibu wa mazingira kutokana na Wakulima kuendelea kukata miti hovyo ili kukaushia Tumbaku hiyo jambo ambalo linaleta athari kubwa kwa mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

Ili kunusuru hali hiyo wataalamu wa kilimo mkoani humo  wakishirikiana na Taasisi ya Utafiti wa zao la Tumbaku, TORITA, wameshauri wakulima wa zao hilo kuanza kutumia mabani ya kisasa na majiko yanayotumia kuni kidogo pamoja na mashina ya Tumbaku baada ya mavuno ambayo yanapatikana kiurahisi.

Kaimu mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya TORITA, Amon Philipo,  ameeleza wamefanya tafiti ya mabani hayo ambayo yanauwezo wa kutumia kuni chache kuliko mabani ya kizamani.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa huo, DR. Philips Mtiba, ametoa ushauri kwa wataalamu kuangalia zaidi matumizi ya majiko hayo ili kumsaidia mkulima kupunguza muda wa kukaa jikoni.

Miongoni mwa wakulima wa Tumbaku mkoani humo Pius Gabriel na Leonard Kushoka, wamekiri majiko hayo yanapunguza gharama ya matumizi ya kuni, na kuiomba Serikali kusimamia mpango huo ili kupunguza uharibifu wa misitu.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>