Published On: Fri, Apr 28th, 2017

WATOZWA FAINI YA UHARIBIFU WA MAZINGIRA

Share This
Tags

Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC  limewatoza faini ya jumla ya shilingi milioni 20 wawekezaji wawili wa kilimo na ufugaji  wilayani Kilolo mkoani Iringa kwa makosa ya kuendesha shughuli zao bila kufanya tathmini ya uharibifu wa mazingira.

Adhabu ya NEMC imeyakumba mashamba ya mifugo ya Tomy Dairies na lile la Ndoto yaliyopo kata ya Ihimbo.

Mwanasheria wa NEMC amesema sheria lazima zifuatwe ili kulinda mazingira.

Mmiliki wa shamba hilo la Tomy amepewa muda wa wiki moja na Kikosi kazi cha kuokoa ikolojia ya Mtoa Ruaha na kung’oa migomba iliyopandwa ndani ya eneo la chanzo cha maji cha Mto Ruaha Mdogo.

Hata hivyo wamiliki wa mashamba hayo wamekiri mapungufu waliyo nayo ambapo  wamesema hawakupewa mwongozo tangu awali.

Aidha wametakiwa kuvitunza vyanzo vya maji vilivyopo ndani ya maeneo yao kwa faida ya vizazi vijavyo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>