Published On: Mon, Apr 10th, 2017
Business | Post by jerome

WAKULIMA WASHAURIWA KULIMA MAZAO YA MUDA MFUPI.

Share This
Tags

Kukosekana kwa usimamizi thabiti wa Misitu imekuwa moja ya mambo yanayochangia uharibifu wa Misitu kutokana na watendaji waliopewa dhamana ya usimamizi kutowajibika ipasavyo katika kuchukuwa hatua kwa waharibifu wa Misitu.

Hayo yamebainishwa Mjini Morogoro na Afisa Programu wa Mradi wa kujengea uwezo jamii kuhusu usimamizi shirikishi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ECOPRC kutoka taasisi ya MJUMITA Bwana Elias Monga wakati alipokuwa akizungumza na Clouds Tv kuhusu hali ya misitu.

Amesema kuwa baadhi ya watendaji wamekuwa wakikaa maofisini na kusubiri kupewa ripoti pasipo kuwa na tabia ya kutembelea maeneo ya misitu kujionea namna inavyosimamiwa au kuharibiwa.

“Unajua utawala mbovu ndio chanzo cha misitu yetu kuendelea kupotea, yani ni kama viongozi wamejisahau, kama hali itaendelea hivi misitu itaendelea kupotea kila kukicha, viongozi watoke maofisini” Alisema Monga.

Kwa upande wake meneja mradi huo wa ECOPRC Bwana Almas Kashinde ametaka kuwepo kwa rasilimali watu wa kutosha watakaopewa jukumu la kulinda misitu ili kuhakikisha wavamizi wa misitu hawapati mwanya wa kuingia misituni.

Baadhi ya misitu imevamiwa na wananchi kwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo, ufugaji, uchomaji holela wa mkaa na ujenzi wa makazi ndani ya misitu kinyume na sheria kutokana na uzembe wa baadhi ya watendaji.

Mratibu wa Mradi huo Richard Giliba amesema Tayari Mradi wa Mradi wa kujengea uwezo jamii kuhusu usimamizi shirikishi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ECOPRC unatekelezwa kwatika wilaya 12 tanzania bara na Zanzibar na umeanza kuleta matokeo chanya baada ya wananchi kuelimishwa.

“Wakati tunaenda watu walikuwa hawatuelewi na misitu ilikuwa ikiharibiwa sana, lakini tangu tuwapatie elimu tunaona wananchi wanaendelea kubadilika.

Mradi wa kujengea uwezo jamii kuhusu usimamizi shirikishi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi ECOPRC unatekelezwa na mashirika mbalimbali ikiwemo MJUMITA,Chuo kikuu cha kilimo sokoine, Chuo kikuu cha misitu OLOMOTONYE chini ya ufadhili wa serikali ya Norway.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>