Published On: Mon, Apr 24th, 2017
Business | Post by jerome

WAFANYABIASHARA MWANZA WALIA NA VYOO

Share This
Tags

Wafanyabiashara wa mnada wa Kishiri Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza wahofia usalama wa Afya zao kwani katika eneo hilo hakuna huduma muhimu ya vyoo na maji hali inayowalazimu kujisaidia vichakani huku ikidaiwa kuchangia uharibifu wa mazingira ya eneo hilo.

Mara nyingi wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga Mkoani Mwanza huzunguka katika maeneo mbalimbali ya minada inayofanyika kila siku za wiki ikiwa ni sehemu ya kujipatia riziki kutokana na biashara zao hizo.

Mkurugenzi wa Halmashauriya jiji la Mwanza KIOMONI KIBAMBA amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kuwaomba wawekezaji kuokoa jahazi hilo.

Mnada huo hufanyika kila ifikapo jumamosi ya kila wiki.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>