Published On: Wed, Apr 26th, 2017

UGONJWA WA AJABU WAUA WATU NCHINI LIBERIA

Share This
Tags

Wizara ya afya nchini Liberia imetangaza kuwa inafanyia uchunguzi sampuli za damu kutoka kwa watu nane ambao wamefariki dunia kutokana ugonjwa usiojulikana katika Eneo la Sineo kilomita 350 kusini mashariki mwa mji mkuu Monrovia.

Msemaji wa wizara ya afya Sorbor George, amesema kuwa jitihada za kuwaokoa waliofariki dunia zilishindwa.

George aliongeza kuwa watu wengine watano wanaoonyesha dalili za ugonjwa huo wamelazwa hopsitalini.

Karibu watu 5000 walifariki nchini Liberia kutokana na ugonjwa wa ebola mwaka 2015 wakati utawala ulikosolewa kwa kutochukua hatua za haraka kukabiliana na ugonjwa huo hatari.

Lakini hakuna ripoti ikiwa watu hao walifariki kutokana na Ebola na taarifa kutoka eneo hilo zinasema watu hawakuwa na dalili za na ugonjwa wa Ebola.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>