Published On: Tue, Apr 11th, 2017
World | Post by jerome

Trump kuiuzia Nigeria ndege za kukabiliana na Boko Haram

Share This
Tags

Utawala wa Trump una mipango ya kuuza ndege za kivita kwa Nigeria licha ya kuwepo wasiwasi unaohusu ukiukaji wa haki za binadamu kufuatia shambulizi la ndege ambalo liliwaua raia kadhaa mwezi Januari.

Ndege aina ya A-29 Super Tucano, zitauzwa kwa Nigeria kusaidia kulipiga vita kundi la kiislamu la Boko Haram, afisa mmoja wa Marekani alisema.

Makubaliano hayo ambayo hayajathibitishwa rasmi yatahitaji kuidhinishwa na Congress.

Harakati za Boko Haram zimesababisha zaidi ya watu milioni mbili kukimbia makwao.

Makubiano hayo yanayotajwa kuwa ya thamani ya dola milioni 600 yaliafikiwa na utawala wa Obama, lakini yakakwama wakati yalistahili kupelekwa mbele ya Congress, baada ya kisa kibaya kilichowahusu wanajeshi wa Nigeria.

Karibu watu 90 wengi wanawake na watoto waliuawa mwezi Januari wakati ndege ya jeshi la Nigeria, iliposhambulia kambi iliyo kaskazini mashariki mwa nchi iliyokuwa ikiwahifadhi maelfu ya watu waliokuwa wamewakimbia Boko Haram.

Shughuli ya ugavi wa chakula ilikuwa ikiendelea wakati wa shambulizi hilo.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>