Published On: Tue, Apr 11th, 2017
World | Post by jerome

Thabo Mbeki aunga mkono wapinzani wa Zuma

Share This
Tags

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Thabo Mbeki amewataka wabunge wa chama cha ANC kutenda yatakayowafaa raia na sio kile kitakachofaidisha  chama, wakati wa kujadili mswada wa kutokuwa na imani na rais Jacob Zuma, wiki ijayo.

Wito wa Mbeki huenda ukawakera wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga mswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.

Upinzani unadai kuwa Zuma ni mfisadi na kuwa alimfuta kazi Pravin Gordhan kama waziri wa fedha, licha ya kuwa Gordhan aliheshimika sana.

Wanasema nia ya Zuma ilikuwa kuchukua usukani katika wizara ya fedha.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>