Published On: Tue, Apr 11th, 2017

SUA KUMUENZI SOKOINE KWA MITI 5000

Share This
Tags

UHARIBIFU wa mazingira  unaotokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu   umekuwa ukisababisha  mabadiliko ya tabia ikiwemo ukame,matetemeko na mafuriko na kwamba  takribani hekta  laki tatu na nusu hupotea kila mwaka kutokana na ukataji miti unaochangiwa  kilimo kisichozingatia hifadhi ya mazingira ,ukataji mkaa,kuni na usafishaji mashamba  kwenye misitu .

Katika kuunga mkono jitihada za kukabiliana na uharibifu wa mazingira  Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) cha mkoani Morogoro kinatumia kumbukumbu ya miaka 33 ya  kifo cha  aliyewahi kuwa waziri mkuu wa awamu ya kwanza  Edward Moringe Sokoine kupanda miti 5000 kwenye eneo la chuo hicho  ambapo  katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais na mazingira Prof. Faustine Kamuzora anatumia zoezi hilo kuwaasa wananchi , taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuendeleza jitihada za kutunza mazingira .

Kwa upande wake makamu mkuu wa chuo cha Sokoine   Prof. Gerald Monera amesema zoezi hilo ni la wiki nzima likiambatana na maonyesho mbalimbali ya shughuli za chuo huku meya wa manispaa ya Morogoro bw. Paschal Kihanga akiusisitizia  uongozi wa chuo hicho kuendeleza jitihada za kupambana na uharibifu wa mazingira kwani  litasaidia kuendeleza  jitihada za kupambana na changamoto hiyo.

Nao wananchi na wanafunzi wa chuo kikuu cha Sokoine walioshiriki kwenye  kumbukumbu ya Kifo cha aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Moringe Sokoine kwa kupanda miti na kushiriki kwenye maonyesho ya shughuli zinazofanywa na chuo KIkuu hicho nao akiwemo sista Helena Mrema kutoka shirika la wamisonari la Wafransisko na mwanafunzi wa SUA bw Mohamed Sadcik  wakawa na haya ya kueleza.

Zoezi hilo la upandaji miti limeenda sambamba na ufunguzi wa maonyesho ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na SUA ambapo pia katika wiki ya  kumbukumbu ya kifo cha aliyewahi kuwa waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine  kutafanyika mhadhara utakaoendeshwa na waziri  wa Kilimo,mifugo na Uvuvi Dr Charles Tizeba ukaokuwa na kauli mbiu Matumizi ya kilimo zana kwa maendeleo  nchini kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>