Published On: Thu, Apr 13th, 2017

SOKOINE BADO HAJAZINGATIWA IPASAVYO NA VIONGOZI WA SASA.

Share This
Tags

Katika kuadhimisha Kumbukumbu ya Kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Hayati EDWARD MORINGE SOKOINE, imeelezwa kuwa mengi aliyoyasimamia na kuyaamini kwa maslahi ya Wananchi, hayapewi uzito kama ilivyokuwa wakati wa uhai wake.

Kauli hiyo imetolewa na Mwandishi Nguli na Mkongwe wa Vitabu nchini, na Mhadhiri wa Chuo Kikuu huria cha Tanzania, Prof EMMANUEL MBOGO wakati akitolea ufafanuzi juu ya namna alivyopata wazo la kuandika tamthilia ya Morani, kupitia maisha ya Hayati SOKOINE wakati wa uhai wake.

Prof MBOGO amesema akiwa tayari amekusanya taarifa mbalimbali kwaajili ya kuanza kuandika kitabu hicho, alifanya safari kurudi chuoni huko nchini Ujerumani wakati huo Marehemu SOKOINE akiwa bado yuko hai.

” Nilipofika Ujerumani katika Chuo nilichokuwa nasoma walikuja wanafunzi wenzangu, wakaniambia walikuwa wanataka kujua mengi kuhusu Tanzania, lakini wakaniambia kuwa walikuwa na Mkutano kuhusu kifo cha SOKOINE, nikashituka kwasababu nilimwacha akiwa hai” Anasimulia Prof MBOGO.

Kisha Prof EMMANUEL MBOGO ameongeza kuwa wengi wakisoma kitabu cha Morani ambacho muhusika wake mkuu ni Dongo, wanahisi kuwa yule ni SOKOINE la hasha ila nilitumia maisha yake kuandaa hicho kitabu.

Mwandishi huyo Nguli wa Vitabu nchini amesema kwa sasa mambo mengi aliyosimamia kiongozi huyo hayapewi uzito ipasavyo, kama ilivyokuwa wakati wa uhai wake jambo ambalo anashauri lipewe uzito ikiwemo kuandaa Makongamano kuhusu maisha ya Kiongozi huyo.

EDWARD MORINGE SOKOINE alipata kuwa Waziri Serikali ya awamu ya kwanza katika vipindi viwili tofauti kabla ya kufariki Aprili 12, mwaka 1984 kwa ajali ya gari eneo la Wami-Dakawa, Wilayani Mvomero, huko Mkoani Morogoro.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>