Published On: Mon, Apr 10th, 2017

SERIKALI YAELEZA MKAKATI WA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU.

Share This
Tags

Serikali imesema kuwa inafahamu changamoto ya uwepo wa magonjwa ya kifua kikuu na Silicosis katika maeneo ya wachimbaji wa Madini. Kwa upande wa Kifua Kikuu inakadiriwa kuwa tatizo hilo ni kubwa ikilinganishwa na hali halisi katika maeneo mengi.

Kwa upande wa Silicosis kumekuwepo na ripoti za wagonjwa wachache katika hospitali za Serikali ikiwemo Kibong’oto ambao ni wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt. Khamis Kingwangalla amesema Serikali kupitia Halmashauri zilizo katika maeneo ya migodi imeanza kuweka mikakati ya kudhibiti magonjwa haya na pia kutoa elimu kwa wachimbaji namna ya kujikinga na vumbi na kutumia njia sahihi za uchimbaji.

Ameongeza kuwa Serikali itaongeza wigo wa huduma katika vituo vya afya kwenye maeneo yaliyoathirika, hususan Mkoa wa Geita ili vituo viwe na uwezo wa kuchunguza na kutibu magonjwa hayo na kuwajengea uwezo wataalamu wa Afya katika kuhudumia wagonjwa katika maeneo ya migodi.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>