Published On: Wed, Apr 26th, 2017

RAIS MAGUFULI NA RAIS MSTAAFU KIKWETE NDANI YA MUUNGANO

Share This
Tags

 

 

Rais Magufuli, amekutana na kusalimana na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dokta Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

Akiongelea uwepo wa Rais Kikwete, Rais Magufuli alichomekea mwenzake Kikwete anaonekana kijana, huku yeye akionekana Mzee kutokana na majukumu mazito ya Nchi yanayomkabili ya kuipeleka Tanzania mbele katika Agenda za maendeleo.

Awali Kabla ya Rais Magufuli, kutoa hotuba yake, Maadhimisho hayo yalipambwa na Burudani Mbali mbali kutoka kwa Wasanii tofauti tofauti

Sherehe hizo za Muungano zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na wajane wa viongozi waasisi wa Muungano mke wa hayati Mwalimu Julius Nyere Mama Maria Nyerere na hayati Abeid Aman Karume, Mama Shadya Karume, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, na viongozi wa chama na serikali.

Kauli mbiu ya Sherehe za Muungano mwaka huu ni ”Miaka 53 ya muungano,Tuuulinde na kuuimarisha, Tupige vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii”

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>