Published On: Thu, Apr 13th, 2017

RAIS MAGUFULI AZINDUA UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE.

Share This
Tags

Rais wa Tanzania DR.JOHN MAGUFULI ameweka Jiwe la Msingi la uzinduzi wa Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na kuagiza kipaumbele cha ajira katika kazi za ujenzi huo kutolewa kwa wazawa.

Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya Tani 30 na uwezo wa kwenda mwendo wa Kilometa 160 kwa saa hali inayoelezwa kusaidia sekta ya usafiri nchini.

Rais DK.MAGUFULI akatumia uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi huo kutaka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa muda.

” Wakandarasi hakikisheni kazi hii inakamilika mapema zaidi ikiwezekana hata kabla ya miezi hiyo 30, ili Watanzania waanze kuitumia huduma hii”

Ujenzi wa Reli hiyo unatarajiwa kugharimu zaidi ya Shilingi Trillion 2.7 ikiwa ni fedha zitokanazo na kodi ya wananchi ambapo Rais MAGUFULI ametaka kipaumbele cha ajira kuanza na wazawa.

Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amesema baada ya kumaliza awamu ya kwanza inayoishia Morogoro, baadae ujenzi huo utafika hadi mikoa ya Dodoma na Mwanza.

Ujenzi wa Reli hiyo utakuwa chini ya wakandarasi kutoka kampuni mbili za mataifa ya Uturuki na Ureno.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>