Published On: Tue, Apr 11th, 2017

NDOA ZA MAPEMA KWA KUTOJUA KUSIMA NA KUANDIKA TANGA!

Share This
Tags
Wananchi wa kijiji cha Ronjo kata ya  Duka-Maforoni wilayani mkinga mkoani Tanga wanakabiliwa na ongezeko la watu wasiojua kusoma na kuandika kutokana na kijiji hicho kukosa shule ya msingi hali inayopelekea watoto wa kike kuolewa wakiwa na umri mdogo.
Kamera ya clouds TV imetua kijiji hapa na kuwanasa walimu na wanafunzi wakiwa darasani, ndani ya darasa hili kunamchanganyiko wa wanafunzi wa darasa la awali, la kwanza na la pili , walimu hawa wamesoma elimu ya watu wazima  na kuishia darasa la nne na kupata jukumu la kufundisha ambapo alama ya kuzidisha anasema jumlisha, ubao wa makaratasi na ukuta.
Martin  Oyaya  ni  mzee wa boma kijiji cha Ronjo  ana jumla ya wanawake 11 na watoto 60  amesema jamii ya  kimasai huongeza idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika  katika kipindi hiki cha sayansi na teknolojia , ambapo katika harakati ya kukabilia na tatizo hili wanafunzi humaliza masomo wakiwa darasa la pili huku wasichana wakiishia  kuolewa.

Aidha   Clouds  amepata furusa ya kuzungumza na  mabinti walio olewa mara baada ya kumaliza kumaliza darasa la pili  wakiongea kwa uchungu huku wakijutia kutopata elimu wanasimulizi za kusisimua.
Kwa upande wa wanafunzi wanaosoma darasa la pili  walimu waliojitolea  kusomesha watoto hao katika jengo la kanisa KKKT  Ronjo wameonyesha kiu yao kielimu na kuiomba serikali kuwatazama kwa jicho la huruma.
Mwenyekiti wa shule hiyo amekili adha wanayopata wanakijiji hao  kutokana na ukosefu wa  huduma ya kielimu kijijini hapo ambapo  uongozi wa kanisa la KKKT horohoro   umeamua kutoa kanisa ili kunusuru watoto hao wapate elimu japo kujua kusoma na kuandika.
Kijiji cha Ronjo kipo kilometa 26 kutoka barabara kuu ya Tanga – Horohoro, kabila linaloishi  hapa ni watu jamii ya wafugaji yaani wamasai, kwa kipindi kirefu kabila hili limekuwa nyuma kielemu kutokana na utamaduni wa kuhamahama kwa kutafuta malisho ya mifugo.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>