Published On: Tue, Apr 25th, 2017
Business | Post by jerome

MKUU WA WILAYA KALIUA LAWAMANI

Share This
Tags

Wafanyabiashara wa wilaya ya Kaliua wamemlalamikia mkuu wa wilaya hiyo ABEL BUSALAMA, kwa kuwafungia maduka yao kutokana na mgogoro kati yao na mwenye nyumba ambaye walikubaliana kimkataba kwa kufuata taratibu za mpangaji.

ABDALAH HEMEDI na HAMISI PAMBAKALI ni baadhi ya wafanyabiashara waliofungiwa maduka yao na mkuu wa wilaya, wakisema kinachowasikitisha zaidi ni kuambiwa kwamba mkataba huo hautambuliki wakati walikubaliana na mmiliki wa nyumba hiyo kukaa kwa miaka kumi na moja bila kulipa kodi.

Mwenyekiti wa wafanyabiashara Kaliua SAIMON MACHABA na PAUL MACHEBA wamekiri kuonewa kwa wafanyabiashara hao, huku HAMISI PAMBAKALI akitoa ushauri kwa vingozi kuwa makini na maamuzi yao.

Mmiliki wa nyumba hiyo SALEHE SULEMANI KATAGA ambae amekana kuzungumzia suala hilo, huku mkuu wa wilaya hiyo ABEL BUSALAMA akisema alifanya hivyo baada ya kuona kuna uvunjifu wa amani na suala hilo kwa sasa liko mahakamani kwa ajili ya utatuzi zaidi.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>