Published On: Mon, Apr 10th, 2017
World | Post by jerome

MISRI YATANGAZA HALI YA DHARURA MIEZI MITATU.

Share This
Tags

Rais Adbel-Fattah al-Sisi wa Misri ametangaza hali ya dharura ya miezi mitatu baada ya mashambulizi mawili ya mabomu dhidi ya kanisa la Mar Girgis mjini Tanta na kanisa ya Saint Mark mjini Alexandria wakati waumini wakisherehekea Jumapili ya Matawi, na kusababisha vifo vya watu 44 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa. Kundi la IS limetangaza kuhusika na mashambulizi hayo.

Rais al-Sisi amelaani vikali kitendo hicho cha kigaidi na kuwapa pole wanafamilia wa wahanga na kueleza dhamira yake thabiti ya kupambana na ugaidi. Pia ametangaza siku tatu za maombolezo kwa waliouawa.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres pia amelaani mashambulizi hayo na kutaka washambuliaji wafikishwe mapema mbele ya vyombo vya sheria.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>