Published On: Tue, Apr 11th, 2017

Meli ya India yaachiwa na Maharamia Somalia

Share This
Tags

Wanajeshi wa Somalia wamenusuru meli moja ya mizigo ya India, ambayo ilitekwa nyara na maharamia mapema mwezi huu, lakini maharamia hao wamekataa kuwaachia huru wafanyikazi 9 kati ya 11, walipokimbilia usalama wao ufukweni.

Kwa sasa inasemekana kwamba wanazuiliwa katika eneo moja karibu na mji wa Hobyo.

Chombo kiitwacho Al Kausar, ni mojawapo ya meli tatu ambazo zimetekwa nyara katika eneo hilo la upembe wa Afrika ndani ya Bahari Hindi, tangu visa vya mwisho vya utekaji nyara kuripotiwa katika maeneo hayo miaka mitano iliyopita.

Mnamo siku ya Jumapili, mabaharia kutoka Indian, Pakistani na China, waliwanasua wafanyakazi wa Tuvalu- meli iliyosajiliwa ambayo ilikuwa imeshikiliwa  na maharamia.

Wafanyakazi hao wawili waliokolewa wakiwa  ndani ya gari ambalo maharamia waliliacha, baada ya kufukuzwa, hayo ni kwa mjibu wa Mohamed Hashi Arabey, Naibu rais wa jimbo la Galmudug, ameliambia shirika la habari la Reuters.

Baada ya Reuters kuwasiliana na maharamia hao, walisema kuwa wataendelea kumshikilia mwanabaharia huyo, hadi pale mamia ya mabaharia wanaozuiliwa nchini India wataachiwa huru.

Uharamia kwenye maeneo ya maji pwani ya Somalia na Yemen, uliongezeka mara dufu mwaka 2011, huku kukitokea zaidi ya mashambulio 200.

Lakini matendo hayo yamepungua pakubwa katika miaka ya hivi karibuni, baada ya kuongezeka kwa doria inayoongozwa na wanajeshi wa majini kutoka mataifa mbalimbali ya dunia, pamoja na uungwaji mkono wa wavuvi wa maeneo hayo wanaoendesha shughuli zao baharini.

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>