Published On: Wed, Apr 26th, 2017

MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YAONGEZEKA KWA WAJAWAZITO.

Share This
Tags

Uelewa mdogo kwa jamii hasa juu ya  lishe  kwa wajawazito kunaelezwa kuwa chanzo cha kuongeza idadi ya watoto wenye ulemavu katika miaka ya hivi karibuni.

Baadhi ya madaktari na waataamu wa afya kutoka taasisi ya THE SAME QUALITY FOUNDATION (SQF) wamesema kwa sasa idadi ya watoto wanaozaliwa na mgongo wazi,vichwa vikubwa na mdomo sungura imeongezeka.

Peter Mabula ni mkurugenzi wa taaasisi ya SQF ambae anakiri kuwapo kwa matatizo hayo huku akitoa wito kwa wazazi na walezi kuwafikisha hospitali watoto wanaobainika kuwa na matatizo hayo mapema ili waweze kupatiwa matibabu.

Zaidi ya watu mia tano wamejitokeza kupima afya zao jijini Arusha katika zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza na kupewa elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa ya kuzaliwa nayo ikiwa ni mwendelezo wa tamasha la mwaka linaloandaliwa na taasisi ya the Same Quality Foundation.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>