KOCHA MOURINHO PASUA KICHWA MAN U
Kocha wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho ameendelea kutokueleweka kwa namna anayoishi na wachezaji baada ya kuonyesha wazi kuwa hana mipango na beki wa kushoto wa klabu hyo Muingereza Luke Shaw.
Mourinho amesema hajaridhishwa na mienendo yake ukilinganisha na mabeki wengine kama Ashley Young na Daley Blind.
Shaw aliyejiunga na klabu hiyo mwaka 2014 kwa kiasi cha paundi milioni 32, amekuwa akikosa nafasi ya kuwepo hata benchi na Mourinho anaona benchi limejaa kwa sababu ana Darmian, Young na Blind.