Published On: Thu, Apr 13th, 2017
Business | Post by jerome

KITENGO MAALUM CHA UWEKEZAJI CHAUNDWA MWANZA.

Share This
Tags

 

Mkoa wa MWANZA umeunda Kitengo Maalumu cha Uwekezaji kuanzia ngazi  ya Mkoa hadi ngazi ya Halmashauri ili kuwapa fursa wawekezaji wanaokuja kuwekeza mkoani humo.

Mkoa huo ni moja kati ya Mikoa mikubwa iliyoko kanda ya Ziwa VICTORIA ukiwa na zaidi ya  wakazi milioni 2 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.

Ukifika MWANZA utapokewa na mandhali nzuri ya mji wa mawe THE ROCK CITY, Mkoa huu una fursa nyingi  za uwekezaji  katika sekta mbalimbali zikiwemo  Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, madini na Viwanda , lakini burudani za utamaduni nazo hazipo nyuma.

Wadau wa maendeleo Mkoani humo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa JOHN MONGELA wamekutana kujadili namna ya kuufaya Mkoa huu kuwa sehemu ya mkakati wa maendeleo, Ikiwa pamoja na kuwa na Viwanda Viwili kila halmashuri ili kukuza mnyororo wa thamani.

Dokta HASSAN  ABBAS  ni Mkurugenzi wa idara ya habari maelezo nae ameshiriki jukwaa hili la biashara na kuwataka wadau wa maendeleo kuhakikisha kuwa wanaweka mipango yao kwa kuzinmgatia utekelezaji wake.

” Unapoweka mipango yako hakikisha unakuwa mtekelezaji, lakini ukipanga bila kutekeleza hautafanikiwa, hata kwenye Ofisi yetu ya habari maelezo ndio maana tumekuja na kauli mbiu ya tunatekeleza” anasema DK ABBAS.

Maeneo yaliyotengwa kwaajili ya uwekezaji katika Mkoa wa Mwanza na Wilaya zake ni Lwanima, Nyamongolo, Ihalalo, Nyang’omango,Bundilya na Hungumalwa

 

 

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>