Published On: Tue, Apr 11th, 2017

KATUMBA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE KUKOMESHA MIMBA ZA UTOTONI!

Share This
Tags

Wakazi wa Kata ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi wameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya shule ya Sekondari Kenswa ikiwa ni pamoja na kujenga mabweni ya wanafunzi ili kusaidia kuepukana na mimba za utotoni.

Maombi hayo yanafuatia baada ya wanafunzi kukosa mabweni na kulazimika kuishi katika nyumba za kupanga na kukumbana na vishawishi kwa baadhi ya watoto wa kike wakishawishiwa na wanaume kwa kupatiwa vitu vidogo vidogo hali inayopelekea kupata mimba na kukatisha Masomo yao.

Mkuu wa shule hiyo  mwalimu Godfrey Tinga ameeleza kuwa kutokana na ukosefu wa Mabweni shuleni hapo kunapelekea wanafunzi kutembea umbali mrefu na shule hiyo inayohudumia vijiji 16 na kuna wanafunzi zaidi ya 1100.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Katumba Kombo Masatu amebainisha kuwa Baraza la Kata Tayari limeadhimia kuanza Ujenzi wa mabweni katika shule hiyo ili kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi hao.

Aidha Diwani wa Kata hiyo Mhe.Seneta Baraka amethibitisha kuwepo kwa Chanagamoto hiyo Huku akiabainisha kuwa Mchakato unaendelea na Ujenzi utafanyika mara baada ya kukamilika kujengwa vyumba vya madarasa vinavyojengwa sasa.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>