JKT YAISHINDILIA ABC KATIKA LIGI YA KIKAPU DSM.
Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar Es Salaam, RBA imeendelea wiki hii na klabu ya JKT ilishinda kwa pointi 76-68 za ABC, TZ PRISON ikashinda 86-64 dhidi ya Chui siku ya Ijumaa.
Jumamosi Mgulani ilifungwa 44-64 za DB Young Stars, JKT ikashinda 80-57 za Magnet, TZ Prison ikafungwa 64-83 za Mabibo Bullets, Jeshi Stars 76 -35 za TZ Prisons Queens na Vijana wakashinda 63-42 za Kurasini Heat. Jumapili ilishuhudia Ukonga Kings ikishinda 80-57 za Mgulani, Vijana Queens wakafungwa 64-75 za JKT Stars, Pazi wakafungwa 72-83 na ABC.
Mchezo mkubwa ulikuwa kati ya Vijana City Bulls dhidi ya Savio ambao ni wapinzani wa jadi. Ikishuhudiwa na mashabiki takribani 1000 ambayo ni idadi kubwa kutokea kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwa takribani miaka 10 iliyopita. Mchezo ulimalizika kwa Savio kushinda 67-55 za Vijana. Babui Mtambo alifunga pointi 18 kwa Savio huku Mwalimu Herry akifunga 14 kwa vijana.