Published On: Wed, Apr 5th, 2017
Sports | Post by jerome

Fainali ya kombe la ligi ya Ulaya kufanyika mwishoni mwa ligi za mataifa

Share This
Tags

Fainali ya kombe la ligi ya Europa itafanyika baada ya kumalizika ligi za ndani za mataifa ya Ulaya katika msimu kuanzia mwaka 2019 baada ya shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA kuidhinisha mpango wa kufanyika mchezo huo wa mwisho katika mashindano ya pili ya vilabu barani Ulaya katika wiki hiyo hiyo ambapo fainali ya kombe la ligi ya mabingwa inafanyika.

Kwa hiyo fainali ya kombe la ligi ya Ulaya msimu wa mwaka 2018 – 19 itafanyika Mei 29, mwaka 2019, kamati kuu ya shirikisho hilo iesema katika taarifa leo.

Wakati huo huo shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA limetoa wito leo kwa chama kinachoendesha ligi za ataifa ya Ulaya EPFL kuacha msimamo wake wa mapambano kuhusiana na mabadiliko ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

EPFL wiki iliyopita ilitishia katika mkutano mkuu kubadilisha siku za mapambano ya ligi ya mabingwa na ligi ya Ulaya , na kutoa uhuru kamili kwa vilabu kuamua mapambano hayo yafanyike lini.

Posted By

-

Leave a comment

XHTML: You can use these html tags: <a href="" title=""> <abbr title=""> <acronym title=""> <b> <blockquote cite=""> <cite> <code> <del datetime=""> <em> <i> <q cite=""> <s> <strike> <strong>